UN:Raia hawana msaada wa chakula S Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msaada wa chakula

Umoja wa mataifa unasema kuwa mamia ya maelfu ya raia hawana msaada wa kuokoa maisha yao kufuatia kuondolewa kwa msaada wa kibinaadamu nchini humo.

Umoja wa mataifa umesema kuwa makundi ya kimataifa ya msaada yalilazimika kuwaondoa maafisa wao katika jimbo la Unity State kutokana na mapigano makali.

Raia wamewachwa bila chakula pamoja na madawa wakati ambapo hifadhi za chakula zimepungua.

Takriban watu laki moja waliwachwa bila makao wiki iliopita kufuatia mapigano makali kati ya vikosi vinavyomtii rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.