Mahakama yawatetea wahamiaji A Kusini

Image caption Wahamiaji Afrika kusini

Mahakama nchini Afrika Kusini imeizuia kwa mda serikali ya taifa hilo kutowarudisha makwao wahamiaji waafrika 300.

Mawakili wameruhusiwa kushauriana na wateja wao baada ya mamlaka kuwazuia kufanya hivyo.

Mamia ya wahamiaji wasio na vibali wamekamatwa katika msako uliofanyika usiku wiki za hivi karibuni.

Hii inafuatia msururu wa ghasia dhidi ya wageni ambapo watu saba waliuawa.