Risasi zasikika nje ya kasri la rais Burundi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Risasi zasikika nje ya kasri la rais Burundi

Polisi wamelazimika kufyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura Burundi.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Maud Jullien amesema kuwa mamia ya waandamanaji walikuwa takriban kilomita moja kutoka kwa kasri ya rais ndipo wakavamiwa na maafisa wa usalama.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura.

Hii ndio mara ya kwanza kwa waandamanji hao kukaribia kasri ya rais mjini Bujumbura tangu maelfu ya watu kuanza kuandamana kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania kuingoza taifa hilo kwa awamu ya tatu kinyume na mwafaka wa amani wa Arusha.

Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wanakutana hii leo mjini Dar es Salaam kujadili mbinu za kutatua mgogoro wa kisiasa ambao inalaumiwa kwa kusababisha vifo vya watu 20.

Mkutano huo utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo, kwenda Bujumbura wiki iliyopita.

Image caption Polisi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura.

Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo,kusikiliza hoja za viongozi wenzake.

Viongozi hao wanatarajiwa kumshinikiza rais Nkurunzinza kuahirisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi juni.