Mwanamke mweusi ndio malkia wa urembo Japan

Image caption Ariana Miyamoto

Ariana Miyamoto aliingia katika shindano la malkia wa urembo nchini Japan baada ya rafikiye mwenye mchanganyiko wa rangi kujiua.

Na alivumilia unyanyasaji baada ya kushinda taji hilo kwa sababu ya rangi yake.

Licha ya kuzuiwa na rangi yake,Miyamoto aliweza kutumia umaarufu wake kusaidia kupigana dhidi ya ubaguzi kama vile mwanamitindo Naomi Campbell alivyovunja tamaduni katika sekta ya mitindo miaka kadhaa iliopita.

''Nina sumbua sana'', alisema Miyamoto mwenye umri wa miaka 21 aliyezaliwa na mama wa Kijapan na baba mweusi kutoka Marekani.Nilijiandaa kukosolewa''.

Image caption Ariana Miyamoto

''Nitadanganya iwapo nitasema haikuniumiza.Mimi ni raia wa Japan,mimi husimama na kuinamisha kichwa wakati ninapojibu simu.Lakini ukosoaji umenipatia motisha zaidi aliambia AFP katika mahojiano.

''Sikujali shinikizo zozote kwa sababu niliingia katika shindano hilo kutokana na kifo cha rafiki yangu.Lengo langu ilikuwa ni kuwahamasisha watu kuhusu ubaguzi wa rangi'',aliongeza Miyamoto ambaye aliteswa shuleni katika eneo la bandari ya Sasebo karibu na Nagasaki.

Mitandao ya kijamii ilitangaza ushindi wa Miyamoto ,huku wengi wakilalamika kwamba ushindi huo ungemwendea raia mwenye mizizi ya Japan na wala sio mtu mwenye rangi.