kikundi cha uokozi wakijaribu kutafuta manusura wa tetemeko la ardhi nchini Nepal
Huwezi kusikiliza tena

Nepal yazidi kutetemeshwa

Raia wa Nepal wanaendelea kuwa na hofu baada ya nchi hiyo kupigwa kwa mara nyingine na tetemeko la ardhi ikiwa ni siku kumi na saba tu, baada ya tetemeko jingine kubwa kuipiga nchi hiyo na kuua zaidi ya watu elfu nane.

Tetemeko hili jipya limesababisha vifo vya watu zaidi ya arobaini na vifo vingine kumi na saba kutokea kaskazini mwa India.

Hata hivyo kumekuwa na wasiwasi mkubwa wa idadi ya majeruhi wa janga hilo kuongezeka hapo baadaye.

Wanakijiji wanaoishi karibu na eneo la maonesho ya hadhara Mashariki mwa mji wa Kathmandu walishuhudia nyumba zao zikiporomoka kama mwamba milimani .

Watu kadhaa waliopolewa kutoka katika matope yaliyokuwa yamewafunika kwenye magofu ya zilizokuwa nyumba zao. Huko Kathmandu jengo la Bunge la nchi hiyo lilionekana katika runinga likitikiswa kwa kasi kubwa huku majengo ya serikali nchini India yalionekana kuharibiwa vibaya.

Mwandishi wetu Regina Mziwanda ametuandalia taarifa ifuatayo: