Tetemeko jipya Nepal laua watu 60

Image caption Raia wa Nepal wakishangaa matokeo ya tetemeko jipya

Wakati kukiripotiwa mvua kubwa na tetemeko kubwa na jipya nchini Nepal, Wakuu nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo jipya , imepanda na kufikia zaidi ya watu 60.

Wakati huo huo helikopta ya kikosi cha majini cha Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu nane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wenyeji wa jeshi la Nepal.

Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.