Burundi:Rais Nkurunzinza ''apinduliwa''

Image caption Ramani ya kanda ya Afrika Mashariki

20:42 Hakuna uhakika iwapo ndege ya rais Nkurunzinza itaruhusiwa kutua

Image caption Wanajeshi wakitangamana na raia barabarani Bujumbura

20:41 Ndege haziruhusiwi kutua ndani ya uwanja huo

Image caption Wanajeshi na raia Bujumbura

20:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura anasema kuwa taa katika uwanja wa ndege zimezimwa.

Image caption Maelfu ya wafuasi wa ''mapinduzi''

20:31Meja jenerali Godefroid Niyombarekuwa ametangaza kufungwa uwanja wa ndege wa Bujumbura.

Image caption Waandamanaji wakisheherekea

20:30 Meja jenerali Godefroid Niyombarekuwa ametangaza kufungua kwa mipaka yote ya Burundi.

Image caption Rais Nkurunzinza hajulikani aliko

20:29 Kundi hilo limekanusha tangazo la Meja jenerali Godefroid Niyombare kuwa ameipindua serikali ya Nkurunzinza

20:28 Kundi la wanajeshi wanomuunga mkono Nkurunzinza wangali wanadhibiti Ikulu na kituo cha redio ya taifa''AFP''.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

20:27 Duru nchini Burundi zinasema kuwa maafisa wachache wa jeshi wanaomuunga mkono rais Nkurunzinza wamejitokeza

19:00 Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amewataka wahusika wakuu nchini Burundi kuweka uhasama baina yao kando ilikulinda taifa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi waliokuwa wakipigana na waandamanaji wameondoka

18:55 Mwandishi wa BBC aliyeko Dar es Salaam anasema kuwa ndege ya rais Nkurunzinza imepaa ikielekea Bujumbura

18:53 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza kufungwa kwa mipaka

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia Burundi

18:45 Mwandishi wa BBC huko Bujumbura Kazungu Lozy anasema watu wangali wanasheherekea

18:40 Rais Nkurunzinza ameingia ndani ya gari lake na kuondoka mjini Dar es Salaam akionesha dalili kuwa yuaelekea Burundi

Image caption Rais wa Burundi

18:37 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ameamrisha wanajeshi kuzuia rais Nkurunzinza kutua Burundi

18:30 Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya kurejea kutoka Tanzania amesema msemaji wake Willy Nyamitwe.

Haki miliki ya picha ap
Image caption Wanajeshi wanasemekana kuzingira uwanja wa ndege

18:25 Generali Niyombareh ametoa amri kwa majeshi kuungana na kulinda viwanja vya ndege kote nchini humo

18:20 Generali aliyeongoza ''Mapinduzi'' leo asubuhi amewataka maafisa wa jeshi na polisi kufanya kazi kwa pamoja ilikulinda usalama wa nchi hiyo.

Image caption Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare

18:15 Viongozi wa kanda ya Afrika wametaka makundi hasimu kutulia na kukubali hali ya kikatiba Kurejea

18:10 Esipisu amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta anaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wananchi waendelea kusheherekea Bujumbura kufuatia tangazo la ''Mapinduzi''

18:07 Msemaji wa rais wa Kenya Manoah Esipisu amesema kuwa viongozi wanataka hali ya kawaida irejee huko Burundi

18:06 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

Image caption Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza

18:05 Rais amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

Image caption Maafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura

18:01 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.

18:01 Viongozi hao wanakutana dar es salaam kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi

Image caption Rais Uhuru Kenyatta akiwa Tanzania

18:01 Rais Jakaya Kikwete amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:00 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

Image caption Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''

17:55 Msemaji wa rais Nkurunzinza ameiambia BBC kuwa asilimia 95 ya taifa hilo ingali salama na wala hakuna tashwishi.

17:50 Manuari zaidi zaonekana barabarani mjini Bujumbura

Image caption Manuari za kijeshi zingali barabarani mjini Bujumbura

17:45 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.

17:30 Msemaji wa rais Nkurunziza,Willy Nyamitwe ameiambia BBC kuwa rais huyo angali madarakani na kuwa hajaondolewa madarakani

Image caption Raia wakiwazoma maafisa wapolisi ambao awali walikuwa wakikabiliana nao

17:22 Redio ya taifa ya Burundi inasema kuwa rais Nkurunzinza angali Madarakani na kuwa hakujakuwa na ''mapinduzi''

17:20 Maafisa wa jeshi wanaolinda kituo cha taifa cha redio wamewaonya watangazaji wasitangaze kuwa kuna ''mapinduzi''

Image caption Raia wakikumbatiana katika bustani la uhuru Bujumbura

17:05 Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema kuwa waandamanaji wamefululiza hadi kwenye vituo vya polisi na magereza yaliyokuwa na mahabusu waliokamata kwa kuandamana na kuwaachilia huru

17:00 Redio ya taifa inasema kuwa bado rais Nkurunzinza angali madarakani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi ya Burundi wakijaribu kutuliza hali Bujumbura

16:50 Kituo hicho cha redio cha ''African Public Radio'' kinapeperusha tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya rais Nkurunzinza

16:40 Redio iliyokuwa imefungwa na serikali ya rais Nkurunzinza kwa kupeperusha habari za maandamano imefunguliwa upya.

Image caption Raia wanasherehekea ''kupinduliwa'' kwa Nkurunzinza

16:30 Mwandishi wa BBC Cyriac Muhawenay aliyeko Bujumbura anasema raia wanaonekana kuwa na furaha.

16:20 Picha za raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi

Image caption Vifaru vya kijeshi katikati ya mji mkuu Bujumbura

16:08 Watu wanaonekana wakininginia kwenye vifaru vya jeshi

16:05 Afisi ya urais nchini Burundi imetangaza kwenye mtandao wake wa twitter kuwa ''hali ni Shwari''

Image caption Raia wakishangilia ''mapinduzi''

16:00 Majeshi wameonekana nje ya kambi za kijeshi mjini Bujumbura

15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani.

Image caption Raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi Bujumbura

15:55 Mwandishi Sonia Rolley, wa Radio France International anasema kuwa halaiki ya raia wamefika nje ya kituo hicho wakishangilia matukio hayo

Image caption Waandamanaji Bujumbura

15:50 Waandamanaji wanasemekana kuambatana na wanajeshi kuelekea katikati ya mji mkuu wa Bujumbura

15:45 Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.

Image caption Waandamanaji Bujumbura

15:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Maud Julien anasema kuwa Miili ya watu watatu imeonekane katika barabara za Bujumbura

15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.

Haki miliki ya picha
Image caption Raia wanashangilia mjini Bujumbura

15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea Burundi.

15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa jeshi la Burundi wanaonekana wakiweka usalama

15:20 Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.

Haki miliki ya picha
Image caption Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu

15:05 Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madarakani.

Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.

Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.

Image caption Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh

Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.

Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

Image caption Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.

Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''