Nigeria:Taarifa ya mgahawa sio za kweli

Tunaomba radhi kutokana na taarifa ambayo tuliichapisha hapa kuhusu mkahawa mmoja nchini Nigeria.Taarifa hiyo haikuwa sahihi na ilichapishwa bila kuzingatia utaratibu wa BBC. Tumeiondoa taarifa hiyo kwenye mtandao na tayari tumeanza uchunguzi kuthibitisha ni nini kilichosababisha taarifa kama hiyo kuchapishwa.

Tunazingatia kwa thamani kubwa sifa ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kama Idhaa inayozingatia uhakika wa habari zake na msimamo wa kutoegemea upande wowote na ni kwa sababu hiyo tunachukua hatua stahiki kuhakikisha kosa kama hilo halifanyiki tena.

“The story about the Nigerian restaurant which we published here was a mistake and we apologise. It was incorrect and published without the proper BBC checks. We have removed the story and have launched an urgent investigation into how this happened.

The BBC Swahili service’s reputation for accuracy and balance remains of paramount importance to us and we are taking the appropriate steps to insure that mistakes like this do not happen again.”