IS yashambuliwa Iraq,kiongozi mkuu auawa

Image caption Abu Alaa al-Afari anayedaiwa kuuawa na majeshi ya Marekani na washirika wake,kupitia shambulizi la anga.

Waziri wa ulinzi wa Iraqi amesema kwamba kiongozi wa pili wa ngazi ya juu katika mamlaka za kundi la wanamgambo wa dola ya kiislamu IS, ameuawa katika mashambulio ya anga na majeshi ya Marekani kwa kushirikiana na majeshi washirika.

Msemaji wa wizara ya ulinzi wan chi hiyo, ameiambia BBC kuwa Abu Alaa al-Afari aliuawa pamoja na seti kadhaa za wanamgamboa wa dola hiyo katika eneo la Tal Afar lililoko kaskazini mwa nchi hiyo ya Iraq.

Lakini waziri wa mambo ya ndani wa Iraq ametilia shaka juu ya kauli hiyo,nayo Marekani haijathibitisha juu ya kauli hiyo mpaka sasa.

Inaaminika kwamba Al-Afari alichukua madaraka ya kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo la is wiki kadhaa baada ya kiongozi wao mkuu, Abu Bakr al-Baghdadi,kupata majeraha makubwa baada ya kushambuliwa kutokea angani .