Obama na uhusiano wa Falme za Kiarabu

Image caption Rais Barack Obama akiwa na Mfalme wa Saudi Arabia Salman

Rais wa Marekani Barack Obama anaongoza mkutano wa viongozi wa falme za kiarab ambao unalenga kuhakikisha uhusiano baina yao na Marekani na Iran ,na kusisitiza kuwa kuna mganyiko.

Viongozi kadhaa walioalikwa kuhudhuria kwenye mkutano huo waliamua kutohudhuria,akiwemo mfalme wa Saud Arabia Salman.

Kutohudhuria huko kumechykuliwa kama mgomo ama kupuuzwa kwa Obama. Lakini serikali ya Marekani haikuliachilia suala hili lipite hivi hivi tu,imetoa tamko na kusema kuwa wanachukulia suala hilo kama fursa ya kumjua vizuri mfalme huyo wa Saudia aliyetawazwa,sherehe ambazo rais Obama alihudhuria.

Seriali ya Saudi Arabia imekuwa kinyume na ushawishi wa mapango wa nyukilia wa Iran,ambao Rais Obama amejitahidi kuhakikisha unafanikiwa.