Askari wa pande hasimu wakabiliana Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi Burundi

Makundi hasimu ya askari yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.

Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.

Radio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.