Rais Pirre Nkurunziza wa Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Rais Pierre Nkurunziza arejea nyumbani

Rais Pierre Nkurunziza amejerea nchini mwake, baada ya kuwepo kwa jaribio la kumpindua akiwa nchini Tanzania kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa wakijadili mgogoro wa Burundi.

Maafisa wa serikali wanasema kurejea nyumbani kwa Rais huyo sasa ni ishara kuwa jaribio la kumpindua limeshindikana.Wakati Rais Nkurunziza akiwasili taarifa za hivi punde zinasema mmoja wa majenerali waliojaribu kuipindua serikali amekiri kuwa jaribio lao linaonekana kuwa limeshindwa

Na kujua zaidi taarifa za kurejea nyumbani kwa rais Nkurunziza awali John Solombi ailizungumza na Msemaji wa serikali ya Burundi Jevier Abayeho.