Narendra Modi awasili nchini China

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Narendra Modi

Waziri mkuu wa India, Narendra Modi, amewasili nchini Uchina kwa ziara ya siku tatu, akipania kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu barani Asia.

Atafanya mazungumzo na rais Xi Jinping, ambapo mjadala wao pia utagusia taharuki ya muda mrefu mipakani mwa mataifa hayo mawili.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Narendra Modi

India pia inatarajiwa kuzungumzia mipango mikubwa ambayo China inawekeza nchini Pakistan, hatua inayotishia taifa jirani ya India.

Bwana Modi anazuru makavazi maarufu ya Terracotta warriors na pia anatazamiwa kuzuru hekalu la kibuddha la Dashang nyumbani kwao rais wa China katika jimbo la Shaanxi.