Wafanya mzaha kuhusu alipo Nkurunziza

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza

Wakati raia wa Burundi wakiwa wanasubiri Rais wao Pierre Nkurunziza kulihutubia taifa baada ya kurejea nchini kwake kufuatia jaribio la Mapinduzi lililoshindwa,baadhi ya watu kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika wametupa picha nyingi za mizaha zinazoonyesha wanamtafuta Rais huyo katika mazingira yasiyo ya kawaida kama vile ndani ya majokofu na chini ya viti.

Rais Pierre Nkurunziza amedai kuwa amesharejea nchini mwake baada ya kukwama nchini Tanzania kutokana na tishio la usalama kufuatia jaribio la mapinduzi.

Viongozi watatu walioendesha jaribio hilo tayari wameshakamatwa huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kuwa zaidi ya watu 100,000 wameikimbia nchi hiyo kwa hofu.

Watumiaji wa mtandao wa Twitter kutoka pande mbali mbali barani Afrika usiku kucha wamechangia mara 2000 katika hashtag, iliyosema "Where is Nkurunziza"

Image caption Nkurunziza

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa tweeter kutoka mji wa Bujumbura, Kris Nsabiyumva, aliwasilisha ujumbe mara kadhaa akiomba msaada kutoka kwa msanii maarufu wa vikaragosi kutoka Marekani Dora kusaidia kumtafuta Rais Nkurunziza huku akiendelea kumtafuta pia chini ya kochi lake.

Naye mmiliki wa blogu ijulikanayo kama Mr Burundi kwa siri alionekana akiyaambia maua yake kuwa,Shangazi yake kaniambia kuwa Nkurunziza ameonekana eneo la Ngozi na kwamba amemuona kwa macho yake, na kwamba wamempata.