Wahamiaji 800 waokolewa na wavuvi Indonesia

Haki miliki ya picha AP
Image caption wahamiaji wa Indonesia

Zaidi ya wahamiaji mia nane wamewasili katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia baada ya kuokolewa na wavuvi mashua yao ilipokuwa ikizama.

Ripoti zasema kuwa mashua nyingine ilirejeshwa Indonesia na jeshi la wanamaji.

Mwandishi wetu anasema kuwa wengi wa watu hao walikuwa wakihitaji matibabu baada ya kukaa baharini karibu miezi mitatu bila maji wala chakula.

Mamlaka za Malaysia imesema kuwa haitaruhusu mashua hiyo kutia nanga katika ardhi yake.