Nkurunziza aonya kuhusu Al Shaabab

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nkurunziza aonya kuhusu Al Shaabab

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu jaribio la mapinduzi la jumatano iliyopita.

Rais Nkurunziza akihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Bujumbura alionya kuwa kuna tishio la shambulizi la kigaidi kutoka kwa kundi la waislamu kutoka Somalia wenye uhusiano na Al-Qaeda , Al Shabaab.

Aliwaambia wandishi wa habari wa kimataifa kuwa tishio hilo la mashambulizi sio tu kwa taifa lake bali pia kwa Kenya na Uganda .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapinzani wake wanashuku ni njama ya kuidhinisha makabiliano makali na waandamani hapo kesho

Hata hivyo mwaandishi wa BBC aliyeko Bujumbura anasema kuwa Nkurunziza hakuzungumzia lolote kuhusu hali ilivyo nchini Burundi wala tishio la mapinduzi dhidi yake.

Aliondoka ghafla akiwa mongoni mwa msafara uliolindwa kikamilifu.

Wapinzani wake hata hivyo wanasema huenda hiyo ni njama ya rais Nkurunziza kuidhinisha makabiliano makali dhidi ya wapinzani wake ambao tayari wameagiza wafuasi wao kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuendelea na maandamano ya kumtaka asiwanie kipindi cha tatu katika kura za urais zitakazofanyika mwezi ujao.

Haki miliki ya picha
Image caption Al Shabab wametishia kuishambulia Burundi kufuatia mchango wake katika majeshi ya AMISOM

Duru kutoka kwa afisi za maswala ya usalama wanje katika serikali ya Marekani na vile vile maswala ya ndani ya serikali ya Uingereza zimekariri tishio hilo la Al Shaabab dhidi ya Burundi kufuatia mchango wake katika jeshi la umoja wa Afrika Amisom huko Somalia.

Marekani tayari imeagiza raia wake kuondoka nchini humo kufuatia tishio la shambulizi la kigaidi mbali na kuzorota kwa hali ya usalama.