3 wauawa katika shambulizi la bomu Kabul

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wawili wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mlipuko kwenye mji mkuu wa Afganistan Kabul.

Watu watatu wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mlipuko kutokea kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji mkuu wa Afganistan Kabul.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga alikuwa amelenga wanajeshi wa kimataifa nje ya lango kuu la uwanja huo wa ndege.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lango hilo hutumika na maafisa wa kijeshi wa kigeni pekee yao.

Watu wengine 20 walijeruuhiwa.

Lango hilo hutumika na vikosi vya kijeshi vya kigeni.

Haijabainika iwapo walikwepa shambulizi hilo au la.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu aliyeshuhudia alilitaja shambulizi hilo kuwa la kujitoa mhanga.

Msemaji wa polisi nchini humo amaiambia BBC kuwa shambulizi hilo lilifanyika karibu na afisi za halmashauri za safari za ndege nchini humo zilizoko nje ya uwanja wa ndege.

Mtu aliyeshuhudia alilitaja shambulizi hilo kuwa la kujitoa mhanga.

Shambulizi hilo linafanyika siku tatu baada ya mwanamgambo mmoja kuwaua watu 14 wakiwemo raia 9 wa kigeni mjini humo.

Kiingilio hicho hutumiwa na na magari ya vikosi vya wanajeshi wa kigeni.