Misri:Marekani yapinga Morsi kunyongwa

Image caption Marekani imeelezea wasiwasi kufuatia kauli ya mahakama ya kumhukumu kunyongwa Morsi

Marekani imeelezea kutoridhishwa kwake na kauli ya kuhukumiwa kunyongwa kwa aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi hapo jana.

Mahakama kuu nchini Misri ilimhukumu Mohamed Morsi na wafuasi wake mia moja kunyongwa kwa kuvamia gereza miaka minne iliyopita.

Marekani inasema kuwa haikuridhishwa kamwe na jinsi upande wa mashtaka uliendesha kesi hiyo ikisema kuwa ilikiuka wajibu wa taifa hilo katika jukwaa la kimataifa.

''Haiwezekani kuwa kesi kama hiyo inayomhusisha rais wa zamani inaendeshwa kwa jumla''

Haki miliki ya picha AP
Image caption Morsi amekataa katakata kutambua uhalali wa mahakama iliopo sasa.

Mahakama hiyo ilimpata na hatia aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi kufuatia kuvunjwa kwa magereza mwaka wa 2011.

Kauli hii ni msumari katika kidonda cha Morsi ambaye alikuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuamrisha kukamatwa kwa waandamanaji waliopinga utawala wake.

Morsi aling'olewa mamlakani na jeshi mwezi Julai mwaka wa 2013 kufuatia kipindi kirefu cha maandamano dhidi ya utawala wake.

Kuanzia hapo chama chake cha the Muslim Brotherhood kimepigwa marufuku huku mamia ya maelfu ya wafuasi wake kukamatwa na vyombo vya dola.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa Misri kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.

Kufuatia uamuzi huo wa kifo , sasa kauli nzima na ruhusa itapatikana tu baada ya uamuzi kutumwa kwa kadhi mkuu nchini humo ambaye sasa ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho iwapo Morsi ataonja mauti au la .

Sheria za nchi hiyo hata hivyo zinamruhusu Morsi kukata rufaa licha ya uamuzi wa kadhi mkuu.

Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kukutu kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasma wa kisiasa baina yake na uongozi ulioko sasa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kukutu kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasma wa kisiasa

Morsi amekataa katakata kutambua uhalali wa mahakama iliopo sasa.

Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa Misri kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru.

Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa afisini.