Raheem Sterling kuipa kisogo Liverpool?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raheem Sterling,mshambuliaji wa Liverpool

Raheem Sterling wa Liverpool anatarajia kumuaga kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers na kuondoka Anfield msimu huu.

Mshambulizji huo katika ligi ya England tayari amekwisha saini mkataba mwingine wa kiasi cha Paund laki moja kwa wiki na kukanusha kuwa yeye hana tamaa na pesa,kama alivyohojiwa na BBC.

Mchezaji huyo anatarajiwa kukutana na Mkurugenzi wake Ian Ayre na Kocha wake Rodgers siku ya ijumaa,ambapo atakuwa tayari kuwaeleza kuwa sasa anapaswa kuiipa kisogo klabu hiyo.

Hata hivyo klabu hiyo ya Liverpool haijataka kusema lolote kwa sasa japo kuwa inaeleweka kuwa bado wanamhitaji mchezaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 20 na ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2017.

Klabu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, ikiwemo Manchester City,Arsenal pamoja na timu nyingine kubwa Ulaya zinamhitaji pia.

Hata hivyo Kaptain wa Liverpool Steven Gerrard akizungumza sikuya Ijumaa wiki iliyopita alimtaka Sterling kubakia katika timu hiyo na kusisitiza kuwa ni vizuri kuwa katika klabu ambayo kocha ana imani na wewe.