Yemen:Serikali yapinga mazungumzo na waasi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption makamu wa rais wa Yemen Khaled Bahah

Serikali ya Yemen iliyoko uhamishoni, haitakubali kufanya mazungumzo ya amani na wanamgambo wa Houthi, hadi pale wanamgambo hao watakapotekeleza maafikiano ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Miongoni mwa muafaka huo, ni kuondoka kutoka katika miji wanayoshikilia na kurejesha silaha walizozichukua.

Hayo yamesemwa leo Jumanne na makamu wa Rais Khaled Bahah.

Shirika la Umoja wa mataifa lilikuwa na matumaini makubwa kuwa makundi yote hasimu nchini Yemen, kwa pamoja na kundi kuu la Houthi na serikali ya Abd-Rabbu Mansour Hadi iliyoko uhamishoni mjini Riyadh, yataungana kwa mazungumzo ya kuleta amani huko Geneva hatimaye mwezi huu ili kujaribu kuleta suluhu na kukomesha mapigano yaliyodumu miezi kadhaa sasa.