Zuma ataka uchaguzi kuahirishwa Burundi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zuma

Rais wa Afrika ya kusini Jacob Zuma amekuwa kiongozi wa hivi karibuni anayetaka uchaguzi wa urais nchini Burundi kuahirishwa.

Akizungumza baada ya mkutano wa kieneo nchini Angola,Bwana Zuma alisema kuwa uchaguzi huo haupaswi kufanyika hadi hali ya amani itakaporudi nchini humo.

Haki miliki ya picha
Image caption Maandamano Burundi

Maandamano yanaendelea katika mji wa Bujumbura kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliopita.

Rais wa taifa hilo amekana madai ya kutaka kulipiza kisasi dhidi ya watekelezaji wa shambulio hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nkurunziza

Wafanyikazi wa mahospitali nchini Burundi awali walielezea kuwa kumekuwa na mshambulizi ya kulipiza kisasi ambapo polisi wamekuwa wakiwajeruhi wanajeshi waliodaiwa kuhusika na jaribio hilo.