Ireland yaamua kuhusu ndoa za jinsia moja

Image caption wapiga kura wajitokeza kwa wingi nchini Ireland ili kuamua kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za watu wa jinsia moja.

Wapiga kura wengi wameripotiwa kujitokeza kwenye kura ya maoni nchini Ireland ya kuamua iwapo ndoa za watu wa jinsia moja zinaweza kuhalalishwa .

Katika sehemu nyingine ukiwemo mji mkuu Dublin na miji mingine, idadi ya wapiga ilitarajiwa kufikia takriban asilimia 60.

Image caption Ndoa za jinsia moja

Wataalamu wengi wa Ireland walio katika mataifa ya kigeni walirudi nyumbani kupiga kura.

Wale wanaounga mkono ndoa za jinsia moja walitarajia watu wengi kujitokeza.

Haki miliki ya picha AFP GETTY IMAGES
Image caption Wapenzi wa jinsia moja wakitoka katika kituo cha kupiga kura

Ikiwa kura hiyo itafanikiwa Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kupitia upigaji kura.

Matokeo yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo.