Raia wa Ethiopia wapiga kura

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn anatarajiwa kushinda uchaguzi huo

Raia nchini Ethiopia wanapiga kura hii leo kwenye uchaguzi wa kwanza mkuu tangu kifo cha kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo aliyekuwa waziri mkuu Meles Zenawi.

Mrithi wa bwana Zenawi Hailemariam Desalegn, anatarajiwa kupata ushindi mkuwa.

Chama chake kimekuwa madarakani tangu mwaka 1991 na uchumi wa Ethiopia uko katika hali nzuri.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Raia wa Ethiopia wakibeba picha ya marehemu Meles Zenawi wakati wa kifo chake.

Hata hivyo wapinzani na makundi ya haki za binadamu wanasema kuwa kutokuwepo na uhuru wa kusema ina maana kwamba uchaguzi huo hautakuwa wa haki.