Wahamiaji:Kaburi la pamoja lapatikana

Image caption Kaburi la pamoja karibu na kambi za wahamiaji

Utawala nchini Malaysia unasema kuwa umegundua kaburi la pamoja karibu na kambi za kusafirisha watu kimagendo zilizoachwa karibu na mpaka kati ya nchi hiyo na Thailand.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa makaburi hayo yaliogunduliwa wiki iliyopita huenda yakawa na takriban miili 100 inayokisiwa kuwa ya wahamiaji kutoka nchini Myanmar na Bangladesh.

Waziri wa masuala ya ndani wa Malaysia aliviambia vyombo vya habari kuwa ameshangazwa kugundua kuwa huenda kambi hizo zimekuwa eneo hilo kwa miaka mitano.

Mapema mwezi huu makaburi kama hayo yanayoaminika kuwa ya wahamiaji yaligunduliwa eneo lililo kusini mwa Thailand.