Duda aelekea kushinda Uchaguzi Polland

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Poland Bronislaw Komorowsk amekubali kushindwa

Rais wa Poland Bronislaw Komorowsk amekubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

Hata hivyo matokeo rasmi hayajatolewa.

Matokeo ya awali yanaonyesha kwamba Komorowski ambaye ni mshirika wa serikali ya mrengo wa kulia, ameshindwa kwa asilimia 53 kwa asilimia arobain na saba dhidi ya mpinzani wake Andrzej Duda.

Matokeo haya hayakutarajiwa na Komorowski na yanachukuliwa kama tahadhari kwa serikali hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa wabunge baadaye mwaka huu.

Haki miliki ya picha Getty AFP
Image caption Andrzej Duda anayeelekea kushinda uchaguzi nchini Poland

Poland imekuwa na uchumi imara katika miaka ya hivi karibuni ijapokuwa wadadisi wa mambo wanasema raia wa taifa hilo wanadai kutonufaika na maendeleo hayo. Rais mpya wa Poland anatarajiwa kuanza kazi Agosti mwaka huu.