B.Faso:mwili wa Thomas Sankara kufukuliwa

Haki miliki ya picha
Image caption Mwili wa Thomas Sankara kufukuliwa leo Burkina Faso

Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unakisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.

Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake.

Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987.

Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.

Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou.

Haki miliki ya picha
Image caption Mjane wa Sankara, Mariam

Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.

Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.

Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.

Familia yake inashuku kuwa huenda mwili huo sio wake.