Mafuriko yaua 18,Texas Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Greg Abbott, Gavana wa jimbo la Texas

Mafuriko yamesababisha vifo vya watu 18 Magharibi mwa Marekani na Kaskazini mwa Mexco.

Wengi wa waliothibitishwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo ni kutoka mpakani mwa Mexco katika mji wa Acuna.

Hata hivyo katika mji wa Texas watu watatu wamearifiwa kufa pia na wengine 12 hawajulikani waliko baada ya makazi yao kusombwa na mafuriko.

Gavana wa Texas Greg Abbott anasema mafuriko hayo yameleta madhara makubwa katika jimbo lake.