FIFA: Blatter asalia Kimya !

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa FIFA Sepp Blatter kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu maafisa wakuu wa FIFA kukamatwa kufuatia tuhuma za ulaji rushwa

Rais wa FIFA Sepp Blatter anatarajiwa kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza siku moja baada ya maafisa wakuu wa shirikisho hilo kukamatwa kufuatia tuhuma za ulaji rushwa.

Wajumbe na viongozi wa mashirikisho kutoka kote duniani wanakutana leo mjini Zurich Uswiss kwa kongamano ambalo kilele chake itakuwa hapo kesho Blatter anapotarajiwa kuchaguliwa tena kuingoza shirikisho hilo kwa muhula wa tano mfululizo.

Kwa kawaida Blatter huwa anawahutubia wajumbe na kuwakaribisha lakini kufikia sasa tayari imeshabainika kuwa

Blatter ambaye uongozi wake unatuhumiwa kwa kuendeleza ulaji rushwa na mlungula hatohudhuria hafla ya madaktari na wanakamati.

JACK WARNER

Msemaji wa shirikisho hilo amesema kuwa ni wazi kwanini Blatter hatohutubia.

Wakati hayo yakijiri aliyekuwa makamu wa Blatter, Jack Warner amekesha kizuizini Trinidad and Tobago baada yake kujisalimisha kwa polisi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wakuu waliokamatwa

Majasusi nchini Marekani wamemuhusisha bwana Warner na tuhuma za kupokea kiinua mgongo cha zaidi ya dola milioni kumi kutoka kwa shirikisho la soka nchini Afrika Kusini.

Kitita hicho kilikuwa kiinua mgongo chake baada ya Afrika Kusini kupewa uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010.

Warner amepinga kufanya kosa lolote sawa na shirikisho la soka la Afrika Kusini.

BRAZIL

Huko Brazil polisi mjini Rio de Janeiro wamevamia afisi za kampuni moja ya mauzo inayosadikika kuwa na ushirika wa karibu na kampuni ya Traffic inayoshtumiwa kwa kufaidi zabuni za kandarasi za FIFA bila kufuata kanuni za utoaji zabuni.

Afisa mkuu katika kampuni hiyo Klefer Sports Marketing,bwana Kleber Leite amekanusha madai dhidi ya kampuni hiyo akisema kuwa atashirikiana na maafisa wanaoendesha uchunguzi huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa makamu wa rais wa FIFA Jack Warner alikesha kizuizini

Tayari mmiliki wa kampuni hiyo Marekani Traffic bwana Jose Hawilla amekiri kufaidika na uhusiano wake na FIFA kinyume cha sheria na amekubali kurejesha dola milioni 15 naye asamehewe.

WADHAMINI WAKUU

Siku moja tu baada ya maafisa wa kitengo cha FBI kupendekeza kushtakiwa kwa maafisa wakuu 14 wa shirikisho la soka duniani FIFA,

mdhamini mkuu wa FIFA kampuni ya VISA sasa imeonya kuwa huenda ikalazimika kutathmini upya uhusiano baina yake na FIFA hususan kufuatia kukamatwa kwa maafisa 11 kwa madai ya ufisadi.

Wadhamini wengine Coca-Cola, Hyundai na Adidas pia wamelezea kutoridhishwa kwao na jinsi mambo yanayvoendeshwa katika FIFA.

Kampuni ya kutengeza magari ya Hyundai, imelezea kushtushwa na madai dhidi ya maafisa wakuu wa FIFA.