Mlipuaji wa kujitoa mhanga awaua 4 Saudia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuaji wa kujitoa mhanga awaua 4 Saudia

Watu wanne wameuwawa baada mlipuaji wa kujitolea mhanga kujilipua nje ya msikiti mmoja wa waislamu washia nchini Saudi Arabia.

Duru zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa, katika mkasa huo uliotokea katika mji wa Dammam, katika jimbo liliko Mashariki mwa taifa hilo.

Dammam ni makao makuu ya jimbo la mashariki, kuliko na waislamu wachache wa Washia.

Juma moja lililopita, watu 21 waliuwawa baada ya mlipuaji wa kujitolea kufa, alipojilipua ndani ya msikiti mmoja wa katika kijiji kimoja jimboni humo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uhasama wa kidini umekuwa ukitokota baina ya madhehebu ya Sunni na Shia kufuatia mashambulizi ya Saudia nchini Yemen

Uhasama wa kidini umekuwa ukitokota baina ya madhehebu ya Sunni na Shia kufuatia mashambulizi ya Saudia dhidi ya Washia.

Taharuki inazidi kuikumba Saudia, hasa baada ya ndege za Saudi Arabia zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya waasi wa kishia wa Huthi, katika nchi jirani ya Yemen.