Tetemeko la ardhi latikisa Japan

Haki miliki ya picha
Image caption Hata hivyo hakuna taarifa zozote za uharibifu wala maafa kufikia sasa.

Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mji wa Tokyo Japan

Tetemeko hilo ambalo linakisiwa kuwa limefikia kipimo cha 7.8 kwenye vipimo vya Ritcher limetokea takriban kilomita 874 kutoka Tokyo kusini mwa Japan.

Kulingana na idara ya uchunguzi wa ardhi tetemeko hili lilitokea saa tano u nusu na lilidumu kwa takriban dakika moja.

Majengo mengi yalitikiswa mjini Tokyo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tetemeko la ardhi latikisa Japan

Hata hivyo hakuna taarifa zozote za uharibifu wala maafa kufikia sasa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa NHK kitengo cha kuzima moto mjini Tokyo wakaazi wa mji huo wamekuwa wakipiga simu kuomba msaada baada ya jamaa zao kujeruhiwa.

Shirika la habari la Reuters limesema kuwa huduma ya shirika la reli ya kuenda kasi ya Shinkansen imeathirika kwa muda baada ya kupotea kwa umeme.

Reli hiyo inahudumia miji ya Tokyo na Osaka.

Magari moshi mengine mjini Tokyo pia yamesimamishwa ilikuwaruhusu mafundi kukagua reli kama iliathirika au la.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasafiri wamesongamana nje ya vituo vya reli wakisubiri ruhusa ya kusafiri.

Wasafiri wamesongamana nje ya vituo vya reli wakisubiri ruhusa ya kusafiri.

Japan ni moja kati ya mataifa ambayo huathirika pakubwa na matetemeko ya ardhi.

Mwaka wa 2011,tetemeko kubwa lenye nguvu ya 9.0 katika vipimo vya Richter ilikisa taifa hilo na kutibua kimbunga kilichopelekea vifo vya zaidi ya watu elfu 20.

Aidha tetemeko hilo lilisababisha kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha kawi ya kinyuklia ya Dai-Ichi katika mji wa Fukushima.