Chama tawala nchini Itali chapata pigo

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Waziri mkuu nchini Italy Matteo Renzi

Matokeo ya kwanza ya uchaguzi nchini Itali yanaonyesha kuwa chama tawala kimepata pigo.

Ijapokuwa chama hicho kinatarajiwa kuibuka kama chama kikuu na kushinda viti vitano kati ya saba ,lakini idadi yake ya kura ilizopata ilikuwa ya chini zaidi ya ilivyotarajiwa na inaonekana kushindwa jimbo la mrengo wa kushoto la liguria.

Waziri mkuu Matteo Renzi amekuwa akitafuta kuungwa mkono ili kuimarisha idara ya leba,elimu na mabadiliko ya kikatiba.

Uchaguzi huo ulikifanya chama kinachopinga uhamiaji kuimarisha ushindi wake huko Veneto eneo la kazkazin.

Vuguvugu la five star pia lilifanya vyema.