Lori la mafuta lawaua watu 70 Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lori la mafuta lawaua watu 70 Nigeria

Karibu watu 70 wamefariki huko mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto.

Police wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali.

Walioshuhudia wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti ndiposa likakosa mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.

Mmoja ya waliokuwa wakishughulika kuwanusuru waliojeruhiwa amesema magari mengine 12 nayo yalishika moto.

Mwandishi wa BBC aliyeko Nigeria anasema mikasa ya ajali zinazohusu magari ya kubeba mafuta hutokea mara kwa mara nchini humo.

Miaka mitatu iliyopita ajali mbaya sana ya moto wa mafuta iliwaua zaidi ya watu 100 huko Niger Delta katika mkasa uliochangiwa na watu kuchota mafuta yaliomwagika baada ya gari kubwa la mafuta kupata ajali.