Polisi wanyanyasaji kuchunguzwa Kenya

Image caption Vikosi vya usalama nchini Kenya

Maafisa wa polisi nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinazoonyesha maafisa wa polisi wakiwachapa viboko raia wa Somalia.

Takriban vijana kumi wameonekana wamelala ardhini huku polisi mmoja akiwawachapa viboko na mwengine akiwa ameshikilia bunduki.

Waathiriwa hao wametambulika kama raia wa Somalia ambao wamevuka na kuingia nchini Kenya kupitia eneo la kazkazini mashariki mwa Kenya.

Picha hizo zilichapishwa katika mtandao wa facebook wa afisa mmoja wa polisi kutoka eneo hilo.