Muziki wa J-Lo wazua hisia kali Morocco

Image caption Jennifer Lopez

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa kiislamu nchini Morocco za kumtaka waziri wa mawasiliano nchini humo kujiuzulu kufuatia Tamasha la muziki lililomuhusisha msanii Jenifer Lopez mjini Rabat ambalo wamelitaja kama kuukosea adabu uma kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.

J-lo kama anavyojulikana alipanda jukwaani ili kushiriki katika tamasha la muziki la Mawazine huku vyombo vya habari vya serikali vikitaja utendaji wake kama wa hali ya juu.

Lakini malalamishi yalianza baada ya J-lo kuonyeshwa katika runinga huku wito wa kujiuzulu kwa waziri huyo ukitolewa.

Hatahivyo waziri huyo amekataa kujiuzulu.