Andy Murray atinga robo fainali

Image caption Andy Murray mcheza tenis wa Uingereza ametinga robo fainali ya michuano ya French Open baada ya kumbwaga Jeremy Chardy

Mcheza tenis wa Uingereza Andy Murray amefanikiwa kumcharaza Jeremy Chardy wa Ufaransa na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya French Open ikiwa mara yake ya tano.

Murray, anayeshika nafasi ya tatu kwa ubora wa wacheza tenisi wanaume duniani, kwa kuanza kumchapa 6-4 3-6 6-3 6-2 katika mchezo uliodumu kwa saa mbili na sekunde 51.

Sasa atapambana na David Ferrer, anayeshika nafasi ya saba kwa ubora, ambaye alimbwaga Marin Cilic 6-2 6-2 6-4. Cilic anashika nafasi ya tisa kwa viwango vya ubora.

Murray, mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa ameshinda michezo yote 14 aliyocheza kwenye viwanja vya udongo kwa mwaka 2015.