Tambi zapatikana na madini hatari India

Image caption Maggy noodles

Maafisa wa mjini Delhi huko India wamepiga marufuku chakula aina ya tambi ziitwazo ''Maggi noodles'' baada ya kufanyiwa uchunguzi na kugunduliwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini hatari aina ya lead.

Tambi hizo za ''Maggi noodles'', ambazo zinatengenezwa na kampuni maarufu ya Nestle ya huko India zilikuwa zikipendwa sana na kununuliwa kwa wingi na walaji wengi .

Kampuni yenyewe imejitetea kuwa vyakula vyao ni salama.

Lakini kufuatia tukio hilo la kupigwa marufuku kwa ''Maggi noodles'' hisa zao zimeporomoka katika soko lao la huko India .