Sokwe hawajambo kwa upishi wa vyakula

Image caption Sokwe akifikiri la kufanya

Wanasayansi kutoka Marekani wana imani kuwa sokwe wana uwezo na akili ya kupika chakula. Wanasayansi hao wamefanya baadhi ya majaribio ambayo yameonyesha kuwa sokwe wanaweza kupika mboga za majani na wana uwezo wa kuhimili kusubiri chakula cha moto.

Hata kama wanyama wengi wana desturi ya kula chochote wanachokipata na kula moja kwa moja. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Harvard wanasema matokeo ya utafiti walioufanya unasema kuwa Sokwe wana uwezo wa kupika na inawezekana suala hili liligundulika muda mrefu uliopita.

Hivyo wanachokihitaji sokwe ni ujuzi wa upishi kwani imedhihirika kuwa wana uwezo wa kuhimili moto.