Vitambulisho vya kielektroniki kutumika nchini Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Vitambulisho vya kielektroniki kutumika TZ

Makubaliano ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliidhinisha matumizi ya vitambulisho vya kitaifa vya kielektroniki kwa ajili ya safari za ndani ya jumuiya. Nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda tayari zimeanza matumizi ya vitambulisho hivyo kwa raia wake ajili ya safari za ndani ya nchi wanachama. Lakini Tanzania, ambayo pia ni mwanachama wa jumuiya bado haijaanza matumizi ya vitambulisho hivyo na utoaji wake unaendelea. Leonard Mubali amefuatilia kinachoendelea na kututumia taarifa ifuatayo.