Watu 5 washtakiwa kwa mauaji ya Garissa

Image caption Garissa

Watu watano wameshtakiwa kwa tuhuma za kula njama za kufanya kitendo cha ugaidi kuhusiana na shambulio lililofanywa na Al Shabaab huko Garissa kaskazini mwa Kenya miezi miwili iliyopita.

Haijawekwa wazi watu hao walihusika vipi na shambulio hilo lililosababisha vifo vya Watu 148 .

Maafisa wa usalama wa kenya walisema shambulio hilo lilifanywa na watu wanne ambao wote walikabiliwa na kuuawa .