Wapiganaji 10 wa Taleban wauawa na IS

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Taleban nchini Afghanistan

Jeshi la Afghanistan limesema wanachama kumi wa kundi la Taliban wameuliwa na wapiganaji wa Islamic State walioko mashariki mwa nchi hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu mauaji hayo yalipatikana kwenya taarifa ya siri kutoka duru za kijeshi ambayo ilitumwa kwa vyombo vya habari kimakosa.

Kuuwawa kwa waTaliban hao kwa kukatwa vichwa na wanamgambo hao wa ISIS kunajiri baada ya mapigano ya wiki kadhaa kati ya pande hizo mbili katika wilaya Achin karibu na mpaka na Pakistan .