Wanawake na wanaume walumbana Saudia

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wasaudia

Wasaudi wamekuwa wakilumbana kwenye mtandao baada ya wengi wao kujitokeza kuchangia ujumbe uliowekwa wiki hii wenye maneno na na nukuu " Don't marry a Saudi man", yaani ole wako uolewe na Msaudi.

Malumbano hayo ya mtandaoni yamewaganya upande mmoja wanaume na upande mwengine wanawake -wengi wakisema vipi uolewe kwenye nchi ambayo kila wendapo lazima usindikizwe na mwanamume mwenye uhusiano nawe wa kindugu.

Wengineo wamewatetea wanaume hao wa kisaudi kama watu wanaojua kutunza utamaduni wa nchi yao.

Wanaume wasio katika ndoa pamoja na wanawake wametengwa nchini saidia lakini huwasiliana bila tatizo katika mitandao nchini humo.