Idadi ya waliofariki Ghana yafikia 175

Haki miliki ya picha epa
Image caption Ghana moto

Takriban watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.

Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na stima.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ghana moto

Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra.

Tarayi Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.

Image caption Moto Ghana

Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.

Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.

Image caption Ghana moto

Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio.