Mwandani wa Saddam Hussein afariki

Image caption Tariq Aziz

Taarifa kutoka wizara ya sheria nchini Iraq imetangaza kifo cha Tariq Aziz aliyekuwa mshauri wa karibu wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Saddam Hussein .

Tariq Aziz amefariki dunia mapema leo akiwa angali jela alikokuwa akizuiliwa tangu alipokamatwa wakati nchi hiyo ilipovamiwa kivita na Marekani iliyoungo'a utawala wa Saddam Hussein.

Tariq Aziz amefariki akiwa umri wa miaka 79.

Alihudumu kama naibu waziri na pia waziri wa mambo ya nje wa serikali hiyo ya Sadam Hussein .