Kituo cha tembo yatima chafunguliwa TZ

Image caption Ndovu

Tanzania imeanzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima mjini Arusha.

Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine.

Hatua ya serikali ya kuanzisha kituo hicho inakuja baada ya utafiti wa serikali kubaini kuwa Tanzania hupoteza takriban tembo 30 kila siku.

Kituo hicho kinatarajiwa kutoa uangalizi kwa tembo wadogo wapatao 40, na watahifadhiwa mpaka watakapokuwa wakubwa na hatimae kurudishwa katika mazingira yao halisia.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC, waziri wa Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amebaini kwamba katika hifadhi ya taifa ya Ruaha pekee, tembo wapatao 12,000 walitoweka katika kipindi cha mwaka mmoja.

Waziri Nyalandu amekiri kwamba kiwango hicho ni kikubwa mno na kwamba kinatia wasiwasi hivyo kuongeza kwamba uchunguzi umefanyika kubaini chanzo cha tatizo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndovu yatima wafunguliwa kituo

Mamlaka maalumu ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha na wanyama walio hatarini, imesema kwamba takwimu hizo zinaashiria kwamba Tanzania ni kitovu cha ujangili huku pembe za ndovu zikisafirishwa kupitia bandari ya Dar es

Salaam kwenda nchi jirani.

Tangu mwaka 2009, angalau tani 45 za pembe za ndovu zinaaminika kusafirishwa kwa njia za magendo kutoka Tanzania.

Ripoti zinasema Kenya hupoteza mabilioni ya dola kila mwaka kutokana na ufisadi.