Papa kufanya ziara ya siku moja Bosnia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Papa Francis

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis anafanya ziara ya siku moja nchini Bosnia ambapo anatarajiwa kutoa wito wa kuwepo amani na uwiano nchini humo.

Ataongoza misa katika uwanja mmoja wa michezo kwenye mji mkuu Sarajevo ambapo pia atakutana na waakilishi wa dini zote ambazo zimekuwa nchini Bosnia kwa karne kadha zikiwemo za waislamu, wakiristo wa orthodox, wakatoliki na wayahudi.

Miaka 20 baada ya kumazika kwa vita kwa wenyewe kwa wenyewe Bosnia imebaki imegawanyika katika misingi ya kidini na makabila.