Pistorius 'kuachiliwa huru mwezi Agosti'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanariadha mlemavu kutoka Afrika Kusini Oscar Pistorius huenda akaachiliwa huru Agosti tarehe 21

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius aliyepatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp huenda akaachiliwa huru tarehe 21 Agosti.

Kwa mujibu wa taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa.

Pistorius alikuwa amefungwa mwaka uliopita kati kesi iliyovutia hisia kali kutoka kote duniani.

Pistorius alimpiga risasi mpenziwe ''akidhaniwa kuwa ni mwizi'' usiku wa siku ya wapendanao.

Kiongozi wa Mashtaka Gerrie Nel alidai kuwa Pistorius alimpiga risasi na kumuua bi Steenkamp baada ya wawili hao kuzozana.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiongozi wa Mashtaka Gerrie Nel ameomba mahakama imuongezee adhabu

Kiongozi wa Mashtaka amekata rufaa ya kuachiliwa kwake na mahakama kuu ya rufaa imeratibiwa kuanza kusikiza kesi hiyo mwezi Novemba.

Bwana Nel anaitaka mahakama hii kumuongezea Pistorius kifungo ijapokuwa mmoja wa jamaa zake Pistorius amedai kuwa mwanariadha huyo atasamehewa kabla ya mwisho wa Agosti mwaka huu.