Watalii 8 'walisababisha' tetemeko la ardhi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mlima Kinabalu

Raia wanne wa kigeni wamefikishwa mahakamani nchini Malaysia kwa kusababisha tetemeko la ardhi.

Raia hao wa kigeni wanatuhumiwa kujipiga picha wakiwa uchi juu ya mlima mrefu zaidi nchini humo jambo lililowakasirisha miungu wao waliosababisha tetemeko hilo lililotimia vipimo vya 5.9 kwenye vipimo vya Richter.

Haki miliki ya picha TWITTER
Image caption Watalii wakiokolewa katika mlima Kinabalu baada ya tetemeko la ardhi

Kisa hicho kimefanyika kabla ya tetemeko la ardhi kutokea katika mlima huo wa, Kinabalu na kuwauwa wakweaji milima kumi na nane.

Baadhi ya raia wa eneo hilo wanalaumu janga hilo la tetemeko la ardhi kwa matendo ya raia hao ambao wameshtumiwa kutoheshimu mila na tamaduni za wageni hususan kwasababu mlima huo ni mtakatifu.

Maafisa wa serikali wangali wanawatafuta watu wengine 6 wanaokabiliwa na tuhuma zizo hizo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bendera ya Malaysia ikipaa karibu na mlima Kinabalu

Miongoni mwa wale ambao tayari wamefikisha mahakamani ni mwanamke mmoja mwingereza na raia wengine wawili kutoka Canada na mmoja mholanzi.

Mlima Kinabalu wenye kina cha futi elfu kumi na tatu ni maarufu sana miongoni mwa watalii.