Marekani na marekebisho ya sera ya haki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ashton Carter

Marekani imeboresha zaidi sera zake hasa ile ya haki sawa kwa wote, katika majeshi yake na kuondoa katazo ama marufuku ya watu wanaojihusisha na wenye hisia za mapenzi ya jinsi moja kujiunga na majeshi yake.

Naye waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter,,ametangaza mabadiliko hayo ya kisera wakati akikagua gwaride la askari wenye hisia na wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja .

Ubaguzi kwa misingi ya mwelekeo wa jinsia sasa katika jamii sawa na chuki za kidini,ubaguzi michezoni ,umri na jinsia.

Kuanzia sasa wafanyakazi wa kiraia ambao ni waajiriwa katika Idara ya Marekani ya Ulinzi tayari wana kinga na wanalindwa dhidi ya ubaguzi unaoegemea katika msingi wa masuala ya kujamiiana.