Waziri:Waganda wanapenda ngono mchana

Image caption Dk Simon Lokodo,waziri wa maadili nchini Uganda

Matamshi ya waziri wa maadili nchini Uganda kuwa Waganda wengi hujihusisha na vitendo vya kufanya mapenzi hasa wakati wa kipindi cha mlo wa mchana yamezua gumzo kali katika vyombo vya habari nchini humo na katika mitandao ya kijamii.

Simon Lokodo ameongeza kusema wamiliki wa nyumba za kulala wageni wakamatwe kwa kuwaruhusu wafanyi kazi wanaotoka maofisini wakati wa mchana na kwenda kula uroda vyumbani humo.

Wengi wanakiri kuwa tetesi hizo zimeenea nchini humo kwamba wengi wa wafanyikazi hutumia fursa ya mapumziko ya mchana kujihusisha na vitendo vya ngono na makahaba au wapenzi wao wa pembeni.

Baadhi wanaunga mkono kauli hiyo ya waziri lakini wengine wamemtaka asijihusishe na maisha ya wengine.