Mataifa yaombwa kuungana dhidi ya IS

Haki miliki ya picha EPA
Image caption waziri mkuu wa Australia Tonny Abbot

Waziri mkuu wa Australia, Tony Abbott, ameyaomba mataifa ya Asia-Pacific kuungana ili kusaidia katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi.

Abbot amewaambia mawaziri kutoka kwa mataifa 25 katika mkutano wa kikanda unaofanyika mjini Sydney kuhusu usalama.

Amesema kuwa kundi la Islamic State lina nia ya kutawala dunia, huku akielezea kuwa hilo ni kundi la mauti, lenye mafunzo mabaya ya itikadi kali.

Waziri huyo mkuu ameongeza kuwa Australia imeamua kuzuia raia wa nchi hiyo kujiunga na wanamgambo wa Islamic State

Image caption wapiganaji wa islamic state

Amesema hayo muda mfupi baada ya Rais Barrack Obama kuidhinisha wakufunzi 450 wa jeshi la Marekani, kwenda Iraq.

White House sasa inasema kuwa ina imani mikakati yake ya kutoa mafunzo kwa vikosi vya kiusalama vya Iraq na kuwaingiza jeshini wapiganaji wa kikabila wa Sunni, itafaulu katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa Islamic State.